Nafasi Ya Matangazo

March 13, 2013

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amekipongeza kituo cha utamaduni cha Bujora    kwa kutunza na kuhifadhi  utamaduni wa mtanzania unaolitambulisha kabila la wasukuma jambo litakalosaidia kizazi kijacho kuweza kujifunza utamaduni huo. 
 
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na  Maendeleo (WAMA) alitoa pongezi hizo hivi karibuni alipokitembelea kituo hicho kilichopo wilayani Magu katika mkoa wa Mwanza.
Alisema kuwa kituo hicho kimeonyesha mfano wa kuigwa kwani amejionea na kujifunza mambo mbalimbali ambayo hakuwa anayafahamu hapo awali kuhusiana na kabila hilo jambo la muhimu wahakikishe kuwa wanaendelea kutunza utamaduni wao.
“Kazi mnayoifanya ni nzuri na inatakiwa kuigwa  na watu wengine, hakika kwa  kufanya hivi   mtarithisha utamaduni wenu  kutoka kizazi kimoja hadi kingine, watoto wenu wanatakiwa kujua  mila zao kwani mtu asiye na utamaduni ni mtumwa”, alisema Mama Kikwete .

Akisoma taarifa ya kituo hicho Padre Fabian Mhoja ambaye ni Mkurugezi alisema kuwa kituo kilianza mwaka 1954  kikiwa na lengo la kuhifadhi na kuendeleza tunu bora ya maisha ya watu ili waweze kumfahamu Mungu na kuishi kadiri ya mpango wake kwa kutumia utamaduni.
Alisema kuwa wanajihusisha  na shughuli za kutunza  na kuendeleza urithi wa utamaduni wa mtanzania kwani kupitia kituo hicho wameweza kutangaza utalii na utamaduni ndani na nje ya nchi kupitia ngoma , nyimbo na michezo mbalimbali.
Kituo hicho kimekuwa kikiandaa tamasha la Bulabo ambapo Rais Dk. Jakaya  Mrisho Kikwete amekuwa akichangia ufanikishaji wa tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka na kukusanya watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Posted by MROKI On Wednesday, March 13, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo