Nafasi Ya Matangazo

February 01, 2013

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akimfariji mmoja kati ya abiria waliokua katika Jahazi la Sun Rise, Juma Ali Jaku ,  iliyopata ajali na kuzama  kati ya Tanga na Mkokotoni karibu na Mkondo wa Nungwi, ikiwa imebeba jumla ya abiria 32 kati ya hao 21 wameokolewa na 11 kati yao hadi sasa hawajapatikana. Kushoto kwa Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mh. Pemba Juma Khamis.
Nahodha wa Jahazi ya Sun Rise, iliyozama kati ya Tanga na Mkokotoni, karibu na Mkondo a Nungwi, Abdulla Saleh, akimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, jinsi mkasa huo ulivyowatokea na kuzama baada ya chombo chao kupatwa na dhoruba kali.
*******
ABIRIA 21 kati ya  32 wamenusurika kufa maji baada ya boti ya   Sun rise iliyokuwa ikitoka Pangani Tanga, kwenda Nungwi Unguja, kuzama katika mkondo wa Nungwi baada ya kuzidiwa na mawimbi makali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kamishna Msaidizi, Ahmada Abdalla Khamis, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kunusurika kwa watu hao baada ya kuokolewa na boti zilizotoka Nungwi.

Alisema boti hiyo ilikuwa katika safari zake za kawaida kutoka Tanga kwenda Unguja na ilipofika katika eneo la mkondo wa Nungwi, ilikumbwa na kasi ya mawimbi na kuzama.

“Ni kweli tumepata taarifa ya kuzama kwa boti ikiwa na watu 32 na uchunguzi zaidi kujua chanzo cha ajali hiyo kwa sasa, unafanywa na Polisi,” alisema Kamanda.

Nahodha wa boti hiyo, Abdala Saleh alisema boti hiyo ilipata ajali baada ya kupigwa na mawimbi ya bahari katika mkondo wa Nungwi ambao ni maarufu kwa kuwepo kwa maji yanayovutana.

Saleh alisema juhudi za kujaribu kuepukana na ajali hiyo zilishindikana, ambapo anashukuru msaada wa boti zilizotoka Nungwi pamoja na wavuvi waliokuwepo katika maeneo ya jirani ambao walisaidia.

Kutokana na ajali hiyo, watu watatu wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kaskazini Kivunge wakipata matibabu zaidi baada ya kunywa maji mengi.

Watu 22 walipata matibabu katika Hospitali ya Kivunge na kuruhusiwa kurudi nyumbani. ha kwa jina la Ali Juma.

Hivi karibuni Mamlaka ya Usalama wa Baharini Zanzibar na Mamlaka ya Hali ya Hewa, zilitoa tahadhari kuhusu kuwepo kwa upepo mkali ambapo wavuvi pamoja na wamiliki wa vyombo vya baharini, walitakiwa  kuchukuwa tahadhari.
Posted by MROKI On Friday, February 01, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo