Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka akiwasalimia
wakazi wa kata ya Bunju na Wazo mara baada ya kuwasili katika eneo hilo kwa
lengo la kuzungumza nao ili kutafuta suluhisho la kudumu la mgogoro
wa ardhi kati yao na kiwanda cha Saruji cha Twiga jana jioni.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka akiongea katika
mkutano wa hadhara na maelfu ya wakazi wa kata ya Wazo na Bunju waliojitokeza
kufuatilia maendeleo ya mgogoro wa ardhi kati yao na Kiwanda cha Twiga Cement
ambapo pamoja na mambo mengine amewahakikishia wakazi hao kuwa mgogoro huo
utapatiwa ufumbuzi wa kudumu na kuwaomba kutoa ushirikiano kwake.
Diwani wa eneo la Bunju na Wazo Sharif Exavery Majisafi akiongea na
wananchi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof. Anna Tibaijuka kuzungumza nao.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka
akipitia baadhi ya nakala za ramani zinazoonyesha eneo la Kata ya Bunju na Wazo
pamoja na Kiwanda cha Saruji cha Twiga ambazo ziligawiwa kwa wananchi. Kushoto
ni Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dkt. Silasi Mayunga.
Sehemu ya umati mkubwa wa wakazi wa kata za Bunju na Wazo wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka
(kulia) akiongea na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Saruji cha Twiga (Twiga
Cement) Bw.Pascal Lessoinne (kushoto) mara baada ya mkurugenzi huyo kutoa
taarifa fupi ya maendeleo ya kiwanda hicho na hali ya mvutano wa muda mrefu wa
umiliki wa maeneo baina ya wakazi wa kata za Bunju na Wazo jijini Dar es
salaam.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kijana mmoja ambaye jina lake
halikuweza kupatikana mara moja katikati ya wananchi wenzake akiwa
amevaa kofia ngumu ya waendesha pikipiki wakati wa mkutano wa hadhara wa wakazi
wa kata ya Bunju na Wazo na Waziri wa Ardhi Prof. Anna Tibaijuka kujadili
mgogoro wa ardhi kati yao na Kiwanda cha Twiga Cement. Haikujulikana mara moja
lengo la kuvaa kofia hiyo licha ya mkutano huo kutawaliwa na amani na maelewano
makubwa.
0 comments:
Post a Comment