Jocelyne Maro Miss East Africa 2012/2013 kutoka Tanzania akipunga mkono kwa mashabiki wake mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam akiwashinda warembo wenzake kutoka mataifa mbalimbali ya Ukanda wa Afrika Mashariki na nchi Jirani na Ukanda huo.
Jocelyne Maro Mtanzania wa kwanza kushinda taji hilo toka lililpoanzishwa amejinyakulia zawadi zenye tmamani ya dola za kimarekani 30,000 likiwemo Gari aina ya Toyota Verossa, mara baada ya majaji kumtangaza mrembo huyo ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe huku watu mbalimbali wakimpongeza kwa ushindi wake.
Warembo wakipita jukwaani na vazi la ufukweni.
Warembo wakipita na vazi la Ubunifu.
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia shindano hilo.
0 comments:
Post a Comment