Mratibu
wa mpango wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Wash United Ndugu Femin Mabachi
akiwaelezea waandishi wa habari jinsi watakavyofanya kazi na Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kusaini makubaliano ya msingi katika
kushirikiana kutunza mazingira na usafi. Mpango ambao umelenga zaidi katika
kuendeleza mpira wa miguu kupitia mpango wa TFF wa kuendeleza soka kwa vijana.
Mpango huu wa Wash United unafadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kupitia shirika
lake la maendelea (GIZ). Kushoto kwake ni Mshauri wa mambo ya vyanzo vya maji
na maendeleo ya mazingira wa GIZ Ndugu Falk Negrazus na kulia kwake ni Katibu
mkuu wa TFF Angetile Osiah. Makubaliano hayo yalifanyika katika ukumbi wa
habari wa TFF uliopo katika ofisi zake Karume.
*******
Mpira wa miguu unaweza kufanya nini kuhusu
mazingira na usafi?
Zaidi ya watu bilioni 2.6 duniani wanaishi bila ya kuwa na vyoo. Barani
Afrika, magonjwa ya kuhara yanayosabishwa na ukosefu wa vyoo na usafi ni hatari
zaidi na ndio yanayosababisha vifo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano,
hii ni zaidi ya magonjwa kama Ukimwi, Malaria na surua ikifuatia.
Takwimu
kutoka mashirika ya UNICEF na WHO zinaonyesha kuwa nchini Tanzania zaidi ya
asilimia 90 ya watanzania wanaishi katika mazingira machafu, na asilimia 12
hawana vyoo wala maji. Matokeo yake zaidi ya watoto 24,000 nchini Tanzania
hufariki dunia kila mwaka.
Tabia ya kunawa mikono kwa kutumia sabuni ni njia
rahisi na haina gharama kubwa katika kuzuia magonjwa ya kuhara ambayo haitumiki
sana hapa nchini hasa kwa watoto.
Tatizo kubwa ni kwamba usafi wa mazingira na
afya haupewi kipaumbele katika mawazo ya watu wengi katika vyombo vya habari na
jamii kwa ujumla.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Wash United inafanya kazi kuweka sawa
mambo ya mazingira na usafi katika ngazi zote mahala popote na kuhamasisha watu
kunawa mikono kwa sabuni kila mara. Wash United ni mpango mpya wa kwanza
kutumia nguvu ya mpira wa miguu na mastaa wake katika kuhamasisha unywaji wa
maji safi, mazingira safi na usafi kwa wote barani Afrika na duniani kote.
Katika kukamilisha mpango wake huu Wash United imeungana na wadau mbalimbali
duniani, kwa hapa Tanzania shughuli zinaendeshwa kwa msaada wa shirika la
maendeleo la Ujerumani (GIZ).
Kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania(TFF)
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania
limekubali kushirikiana na mpango wa Wash United katika kuhamasusha tabia ya kutunza
mazingira na usafi kwenye timu za vijana kupitia mradi timu za vijana wa
shirikisho hilo.
Katibu mkuu wa TFF Ndugu Angetile Osiah, leo amesaini mkataba
wa makubaliano kati ya TFF na Wash United. “Ushirikiano kati ya Taasisi ya Wash
United na Shirikisho la mpira wa Miguu ni mpya na wa kujitolea katika sekta ya
mpira wa miguu Tanzania.
Akiongea kuhusu Wash United, mratibu wa Wash United
nchini Tanzania Ndugu Femin Mabachi alisema “Kupitia mpira wa miguu na kwa
kushirikiana na TFF, tunaweza kutunza mazingira na usafi ‘salama’ na kuongeza
uwiano katika kushughulikia mambo haya katika jamii yetu.
Taifa Stars Kuongoza mpango wa Wash United
Kwa kuungana na Wash United, Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litakuwa limejiunga na zaidi ya mastaa 100 wa mpira
wa miguu kama Didier Drogba, Michael Ballack, Arjen Robben, Bayern Munich,
Taasisi za Real Madrid na ile ya Barcelona na pia zaidi ya wananchama 30,000 wa
Wash United duniani kote.
Nahodha wa Taifa Stars Juma Kaseja atawaongoza
wachezaji wenzake kuwa washiriki kwenye mpango huu wa Wash United na kushiriki
katika kampeni nchini Tanzania na duniani kote.
Zaidi ya yote wachezaji wa timu
ya Taifa watashiriki katika shughuli za mchezo wa mpira wa miguu mashuleni
zitakazofanyika hapa nchini zitazokuwa zikiendeshwa na taasisi hizi.
Kama ukitaka kuwa sehemu ya mpango huu kwa
kujiunga na klabu ya Wash United tembelea http://www.facebook.com/WASHUnited
0 comments:
Post a Comment