Vijana
walioshiriki katika uzinduzi wa kinywaji kisichokuwa na kilevi cha
Alvaro kinachotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries,wakigonganisha chupa zao kuashiria ishara ya uzinduzi rasmi wa
kinywaji hicho hapo jana jijini Da es Salaam.
Mmoja
kati ya vijana akicheza”Break Dance”wakati wa uzinduzi rasmi wa
kinywaji kipya kisichokuwa na kilevi cha Alvaro kinachotengenezwa na
Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries LTD.
*******
KAMPUNI
ya Bia ya Serengeti imezindua kinywaji kipya kisicho na kilevi
kinachoitwa Alvaro ambacho kimekuwa kikizalishwa muda mrefu katika nchi
nyingine za Afrika Mashariki. Katika
uzinduzi wa aina yake uliofanyika mwishoni mwa wiki jijin Dar es
Salaam, Meneja wa Kinywaji hicho Anita Msangi alisema kinywaji hicho
kitakidhi wateja wanaotumia vinywaji visivyo na kilevi
Uzinduzi
wa kinywaji hicho uliofanyika katika kumbi za Mlimani City na Quality
Plaza jijini, Dar es Salaam, ulivutia watu kutoka matabaka mbalimbali
ambao walionekana kufuruhishwa na ladha ya kinywaji hicho. Akizungumza
katika sherehe hizo, Bw. Njowoka aliahidi watumiaji wa kinywaji hicho
na vingine vinavyotengezwa na kampuni ya Serengeti kuwa kampuni yake
imejipanga kuona kuwa wateja wanapata bidhaa bora zenye viwango vya hali
ya juu vinavyostahili na kukidhi matakwa ya wateja wake.
Pamoja
na wageni wengi waliofika kwenye uzinduzi huo, sherehe za kuzindua
kinywaji hicho pia zilipambwa na vikundi mbalimbali vya vijana ambavyo
vilionesha uweso mkubwa katika sanaa ya muziki pamoja na kucheza dansi. Kinywaji
cha Alvaro kimekua kikizalishwa kwa muda mrefu katika nchi za Uganda na
Kenya kupitia kampuni mama ya kiwanda cha kutengzeneza bia cha
Serengeti iitwayo East African Breweries Limited.
0 comments:
Post a Comment