Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof.
Makame Mbarawa akijaribu mtambo wa radio kwa kutangaza moja kwa moja (live)
kupitia radio ya jamii LOLIONDO FM mara baada kumalizika kwa hafla ya uzinduzi
rasmi wa radio hio ya jamii iliyowezeshwa kwa ushirikiano kati ya Airtel
na shirika lisilola kiserikali UNESCO katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo
Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha. Waliomzunguka wawakilishi
Airtel na Unesco wakiwa na wenyeji wa kijiji cha Ololosokwani.
Waziri
wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa akifungua jiwe
la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa radio ya jamii ya LOLIONDO FM
wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa radio kijijini Ololosokwani. Uwekwaji wa redio hiyo ya
jamii umezeshwa kwa ushirikiano kati ya Airtel na shirika lisilo la
kiserikali UNESCO katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo
Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha. Kulia ni mkurugenzi wa mawasiliano
wa Airtel Bi, Beatrice Singano na wakwanza shoto muwakilishi wa UNESCO
bi Vibeke Jensen
Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa akisalimiana
wananchi wanakijiji wa kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo
Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha ambapo waziri huyo alikuwa mgeni rasmi
wa katika ufunguzi wa radio ya jamii pamoja na miradi mingine ilikiwemo ujenzi wa nyumba za kimasai za
kisasa
Wadau
wawezeshaji wa radio ya jamii ya LOLIONDO FM wakiwa wamepozi katika
picha ya pamoja na waziri wa Sayansi Mawasiliano na TechnogiaProf.
Makame Mbarawa mara baaada ya uzinduzi wa radio hiyo kijijini Ololoskwani
Kiongozi
******
Maeneo
zaidi ya 10 Tanzania bara na kisiwani kufikiwa Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel kishirikiana na shirika lisilo la kiserikali UNESCO
kwa pamoja wamezindua Radio jamii katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani
Ngorongoro Mkoani Arusha.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na kufanywa na Waziri wa mawasiliano sayansi na technologia Mh Makame Mbarawa.
Mradi wa Radio za jamii ni program maalum inayoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na UNESCO yenye lengo la kusaidia jamii zilizo na changamoto mbalimbali ikiwemo za mila potofu, elimu duni, ukeketwaji, imani za kishirikina, maendeleo duni , ukandamizaji wa wanawake na watoto na hangamoto inginezo.
Maeneo
hayo pia mbali ya kuwa na changamoto huduma za mawasiliano ni duni na
upatikanaji wa huduma za radio kwaajili ya kuelimisha jamii ni
changamoto kubwa.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa radio hiyo, Waziri wa Mawasiliano Sayansi na
Technologia Mh Makame barawa alisema” ninawapongeza Airtel na UNESCO kwa
jitihada zenu hizi katika kuendeleza mawasiliano chini hasa vijijini,
mimi nimefurahishwa sana kuona wadau hawa wanavyojiunga najamii ya
kijijini hapa a kuwaunganisha na sehemu
nyingine za dunia kwa kuweka radio hii ya Loliondo FM ili kuwawezesha upata
habari na taarifa muhimu kwa maendeleo ya taifa”.
Hii
ni fulsa ya pekee kwenu wakazi wa kijiji cha ololosokwani pamoja na
vijiji jirani kuinua shughuli zetu za kiuchumi, kutumia radio hii kutoa
maoni na elimu, Naamini vipindi vitakavyorushwa vitakuwa
vimelenga jamii husika na kuwa chachu ya kuleta ufanisi mkubwa katika mabadiliko na maendeleo kwa ujumla”.
vimelenga jamii husika na kuwa chachu ya kuleta ufanisi mkubwa katika mabadiliko na maendeleo kwa ujumla”.
Aliongeza
Mbarawa Akiongea kwa niaba ya Airtel Mkurungezi wa Mawasiliano Bi
Beatrice
Singano Mallya alisema “Airtel inajisikia furaha kuwa nafasi ya kuchangia maendeleo jamii nchini Tanzania, tunaamini kwamba kupitia redio hii na kwa kupitia mtandao wetu ulioenea zaidi wananchi wamaeneo haya na vijiji takribani 14 vya jirani watanufaika na kuwepo kwa redio Loliondo fm hapa lolosokwani.

Tunategemea
kuona maisha ya ndugu na jamaa zetu wa jamii ya wamasai na wageni waliopo
hapa yakibadilika kwa kasi katika
Nyanja zote” “sasa Wakazi wa ololosokwani watapata nafasi kwa kupitia
radio hii, kutangaza utamaduni
wao, kuboresha na kupata uongozi bora, kutangaza biashara zao na ukuza
soko huku wakitumia huduma ya Airtel money kupata malipo na kuhifadhi
pesa zao kwa usalama zaidi” alisema Singano Singano aliongeza kuwa
“Mbali na Radio tumeweza pia kuwawezesha wakazi wa kijijini hapa kupata huduma ya internet kupitia
Multimedia center tuliyoijenga na kuiwekea mtandao wetu wenye spidi wa
3.75G, Aliongeza
Singano Naye mwakilishi kutoka UNESCO bw,
Ali-amin Yusuph lisema “UNESCO inayofuraha kuona mradi wa radio
unakuwa na kuwafikia wananchi wengi nchini kwa shirikiano wa Airtel,
kuwepo kwa radio hii kutaunganisha wakazi wa Ololosokwani na wale
wa maeneo mengine nchini na dunia kwa ujumla.
UNESCO
tunayo miradi mingi sana ya kusaidia jamii na Mradi wa
Radio hapa Olosokwani umetusaidia kuona maeneo mengine mengi ya kuweza kusaidia jamii hii ya kimasai, leo tunayo miradi mbalimbali tuliyoianzisha hapa ikiwemo Mradi wa Solar (umeme wa jua) ambao utawawezesha akina mama kupata kipato.

Kwa
kupitia mradi huu wakazi wa hapa wamepata sehemu za kuchajia simu zao na
kuweza kufanya shughuli zinazohitaji umeme kwa malipo kidogo”.
“Halikadhalika
tumeweza kurekebisha nyumba za kimasai na kuzifanya ziwe na muundo wa
kisasa unaotoa moshi nje ya nyumba na kuzifanya ziwe na kiwango bora”
Alimaliza kwa kusema mwakilishi kutoka UNESCO bw, Ali-amin Uzinduzi
wa kituo hicho cha radio ijulikanayo kama LOLIONDO FM
uliambatana na ugawaji wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa wanafunzi wa shule mbalimbali kijijini humo kutoka kwa kampuni ya Airtel ikiwa ni kuwahamasisha wanafunzi wengi kupenda fani ya sayansi wakiwa tangu wadogo kitu ambacho kitachangia kuongeza idadi ya wataalamu wa sayansi hapa nchini
Airtel kwa kushirikiana na UNESCO inaendelea na mradi wa radio jamii unaotegemea kufikia maeneo mengi zaidi nchini ikiwemo Sengerema Mwanza, Karagwe Kagera, Chake Chake Pemba, Makunduchi Unguja ,Pangani Tanga, Kyela Mbeya , na Kalama Shinyanga.

0 comments:
Post a Comment