Afisa Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Wakili Ileth Mawala akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya jumla ya flana 130 na Truck Suits 18 zitakazotumika kwenye shughuli ya kukimbiza mwenge Mkoani Rukwa ambayo itaanza tarehe 15-18, Septemba 2012. Mkuu huyo wa Mkoa alishukuru kwa zawadi hizo na kutoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo wa PSPF kwa kuchangia kwenye shughuli za maendeleo Mkoani Rukwa na Taifani kwa ujumla.
Afisa huyo wa PSPF akikabidhi mchango huo kwenye maboksi kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kama inavyoonekana pichani.
Ujumbe ambao upo kwenye flana na truck suits hizo kama unavyosomeka hapo juu. Mbio za mwenge mwaka huu zinabeba ujumbe wa sensa ya watu na makazi pamoja na mabadiliko ya katiba. (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa).
0 comments:
Post a Comment