Nafasi Ya Matangazo

July 19, 2012

Bi. Aziza Mcha,mkazi wa Kijiji cha Mtende, Wilayaya Kusini Unguja akikabidhi karatasi yenye maoni yake kwa Mjumbe wa Tume yaMabadiliko ya Katiba Bw. Mohammed Yussuf Mshamba hivi karibuni katika mkutano uliofanyikakatika shule ya Mtende (Picha na Othman Maulid).
*******
NaMwandishi Wetu, Da es Salaam
Kufuatiaajali ya meli ya Mv Skagit iliyotokea jana, Jumatano, Julai 18, 2012 katikaeneo la Chumbe, Zanzibar, Tume ya Mabadiliko ya Katiba imesitisha Mikutano yaKukusanya Maoni ya Wananchi kuhusu Katiba Mpya iliyokua inaendelea katika Mkoawa Kusini Pemba.

Kwa mujibu wa taarifailiyotolewa jijini Dar es Salaam na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Alhamisi,Julai 19, 2012) mikutano iliyositishwa ni ile iliyopangwa kufanyika kuanzia leo(Alhamisi, Julai 19, 2012) hadi keshokutwa (Jumamosi, Julai 21, 2012) katikamaeneo ya Wawi, Vitongoji,Chanjamjawiri, Pujini, Gombani na Wara.

“Tume imepokea kwa masikitikomakubwa Taarifa ya ajali ya Meli ya MV SKAGIT na imesitisha Mikutano yakukusanya Maoni ya Wananchi kuhusu Katiba Mpya iliyokuwa inaendelea katika Mkoawa Kusini Pemba,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Katikataarifa hiyo, Tume ya Mabadiliko ya Katiba imesema zoezi la kukusanya Maonilitaendelea kuanzia Jumapili tarehe 22, Julai, 2012 na kuwa ratiba ya Mikutanokatika maeneo yaliyositishwa itatolewa baadaye.

 Hatahivyo, Tume ya Mabadilikio ya Katiba imesema katika taarifa yake kuwa mabadilikohaya hayahusu mikutano ya kukusanya maoni inayoendelea kufanyika katika mikoasita (6) ya Tanzania Bara ambayo ni Pwani, Tanga, Dodoma, Shinyanga, Kagera naManyara. 

“Tumeinawaomba wananchi wa Mikoa hii kuendelea kujitokeza kwa wingi na kutoa maoniyao,” imesema Tume katika taarifa hiyo na kuongeza:

 “Tumeya Mabadiliko ya Katiba inatoa pole kwa wafiwa, majeruhi na wote walioguswa naajali hii na tunamuomba Mwenye Mungu azilaze roho za marehemu mahali pemapeponi na majeruhi wote waponekwa haraka,” imesema.
Posted by MROKI On Thursday, July 19, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo