Nafasi Ya Matangazo

June 18, 2012

 Msanii  mahiri wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Wanaume Halisi lenye maskani yake Temeke,jijini Dar es Salaam,Juma Nature akiwarusha baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya NMC, wakati kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ilipokuwa ikizindua huduma yake mpya ya Airtel Jiunge na Supa5 kwa wakazi wa Arusha.
 Mmoja wa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya akiwa amebebwa juu juu na wenzake wakati msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Juma Nature alipopanda jukwaani na kuzikonga nyoyo za mashabiki wake vilivyo jana jioni wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5,uliofanyika  kwenye viwanja vya NMC mjini Arusha.
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya simu za Mikononi ya Airtel-Arusha,Bwa  Bw Stephen Akyoo akimkabidhi simu aina ya Samsung mmoja wa wakazi wa Arusha aitwaye Lucas George mara baada ya kushinda shindano la kughani ,wakati kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ilipokuwa ikizindua huduma yake mpya ya Airtel  Jiunge na Supa5,uliofanyika kwenye viwanja vya NMC mjini  Arusha. Huduma ya Airtel Jiunge na Supa5 ilizinduliwa rasmi hivi karibuni jijini Dar na baadaye kuendelea kuzinduliwa katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuwapa kilicho bora wateja wake popote pale walipo.
 Wakazi wa jiji la Arusha wakiendelea kuhamia na kujiunga kwa wingi  na Airtel.
 .Mmoja wa wasanii anaeitikisa anga ya muziki wa hip hop nchini,anatamba na tuzo mbili za muziki huo huo huo wa hip hop,Roma akiamsha amsha hadhira kubwa ya watu iliojitokeza jioni ya leo kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel,Airtel Jiunge na Supa5,uliofanyika jana kwenye viwanja vya NMC mjini  Arusha na kuhudhuriwa na umati mkubwa watu.
Anajiita Mwamba wa Kaskazini,Msanii mwingine mahiri katika miondoko ya muziki wa hip hop nchini,Joe Makini  akitumbuiza kwenye jukwaa jana kwenye viwanja vya NMC jijini Arusha,wakati kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ilipokuwa ikizindua huduma yake mpya ya Airtel Jiunge na Supa5 kwa wakazi wa Arusha.
Posted by MROKI On Monday, June 18, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo