Mkazi wa Iringa Bw. Philip Gucha akiwa amepanda pikipiki mpya ambayo amejishindia katika promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL, makabidhianoya pikipiki hiyo yalifanyika jana mkoani Iringa mjini.
Kampuni ya Bia ya Serengeti jana imekabidhi zawadi ya bajaji mpya na pikipiki mpya kabisa kwa washindi wa zawadi hizo mkoani Iringa ambapo Bajaji ilikabidhiwa kwa Bw Fadhili Manzi katika mji mdogo wa Mafinga mkoa humo na pikipiki ilikabidhiwa kwa bw………… mjini Iringa ni katika promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti.
Ni wiki ya 6 sasa kati ya wiki 16 za promosheni hiyo ambapo katika droo ya sita iliyochezeshwa hivi karibuni washindi wawili walipatikana ambao ni bw. Deusdedit Tobias Njau 22 kutoka kiboroloni mkoani Kilimanjaro ambaye alijishindia jenereta mpya na Bw. Vicent Lymo 36 kutoka kibosho mkoani Kilimanjaro ambaye amejinyakulia pikipiki mpya kabisa ambayo naye atakabidhiwa zawadi yake siku chache zijazo pindi taratibu za usajili zitakapokamilika.
Makabidhiano hayo yalifanyika jana na kupata kuhudhuriwa na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini huku tukio zima likishuhudiwa na umati mkubwa wa watu ambao walitoa maoni mabalimbali juu ya zoezi zima la promosheni hiyo na kusema SBL inabadilisha maisha ya watanzania wengi hasa vijana jambo ambalo linapaswa kuigwa na makampuni na mashirika mengine hapa nchini.Washindi hao wameishukuru SBL nakuitaka iendelee na moto huohuo.
Akiongea na waandishin wa habari wakati wa kukabidhi zawadi hizo meneja wa masoko SBL mkoa wa Iringa Bw. Philip Gucha amesema washindi hao walipatikana kihalali na kwamba kila mtanzania mweneye sifa zilizoainishwa katika vigezo na masharti ya promosheni hiyo ana haki na uwezo wa kushiriki na kushinda zawadi mojawapo au zaidi kati ya zawadi zilitajwa katika promosheni hiyo “leo tunawakabidhi hawa zawadi zao lakini zawadi hizi ni robot u ya zawadi zite ambazo tunawasubiri ninyi watanzania na wateja wetu wote kujishindia” alisemaGucha na kuwataka watanzania wote wenye mapenzi mema na kampuni ya bia ya Serengeti waendelee kushiriki kwani batahi ya mtu haiwezi kwenda kwa mwingine.
Hii ni droo ya sita wiki ya sita mfululizo ambapo bado takriban wiki 11 sasa ili kuisha kwa promosheni hiyo ya pekee na ya kwanza kutokea hapa nchini ambapo zaidi ya milioni 780 za kitanzania zinashindaniwa kote nchini
Kwa upande wake mshindi wa bajaj bw. Fadhili Manzi amesema kwasasa safari ya maisha yake na familia yake itabadilika kutokana na zawadi hiyo kwani ni sawa na mkulima hodari kuzawadiwa trekta “Sasa wale vijana wenye uwezo wa kuendesha bajaj walete vyeti na leseni zao za udereva wa bajaj ili niwape kazi kwani hii bajaj inaanza biashara haraka iwezekanavyo” alisema Manzi ambaye alionekana kujawa na furaha ya pekee na kutumia fursa hiyo kuishukuru kampuni ya bia ya Serengeti kwa kumwezesha kupiga hatua kubwa kimaisha.
0 comments:
Post a Comment