Nafasi Ya Matangazo

February 08, 2012

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2011 YAPO HADHARANI 
KUYASHUHUDIA GONGA HAPA KUPATA MATOKEO
 
Kwa wasichana kuanza daraja la kwanza ni 1,100; la pili 2,454; la tatu 6,759; la nne 59,600 na sifuri ni 74,667. Wanaoongoza Alizitaja shule 10 zilizofanya vyema katika kundi la shule zenye watahiniwa 40 na zaidi ni St. Francis Girls (Mbeya), Feza Boys (Dar), St. Joseph Millennium (Dar), Marian Girls (Pwani), Don Bosco (Iringa), Kasita Seminary (Morogoro), St. Mary’s Mazinde Juu (Tanga), Canossa (Dar), Mzumbe (Moro) na Ilboru (Arusha).

Kwa shule 10 za mwisho zenye watahiniwa 40 na zaidi ni Bwembwera, Pande Darajani, Mfundia, Zirai (Tanga), Kasokola (Rukwa), Tongoni (Tanga), Mofu, Mziha (Morogoro), Maneromango na Kibuta za Pwani. Aidha, shule 10 bora zenye watahiniwa chini ya 40 ni Thomas More Machrina (Dar), Feza Girls (Dar), Dung’unyi Seminary (Singida), Maua Seminary (K’njaro), Rubya Seminary (Kagera), St. Joseph Kilocha Seminary (Iringa), Sengerema Seminary (Mwanza), Lumumba (Unguja), Queen of Apostles Ushirombo (Shinyanga) na Bihawana Junior Seminary (Dodoma).

Shule goigoi katika kundi hilo ni Ndongosi, St Luke (Ruvuma), Igigwa, Kining’ila (Tabora), Ndaoya (Tanga), Kilangali (Moro), Kikulyungu (Lindi), Usunga (Tabora), Mtu Bubu Day (Dodoma) na Miguruwe (Lindi). Wanafunzi 10 bora ni Moses Swai (Feza Boys), Rosalyn Tandau (Marian Girls), Mboni Maumba (St Francis Girls, Mbeya), Sepiso Mwamwelo (St Francis Girls), Uwella Rubuga (Marian Girls), Hellen Mpanduji (St Mary’s Mazinde Juu), Daniel Maugo (St Joseph Millennium, Dar), Benjamin Tilubuzya (Thomas More Machrina, Dar), Simon Mbangalukela (St Joseph Millennium) na Nimrod Rutatora (Feza Boys).

Wasichana 10 bora ni Tandau (Marian), Maumba (St Francis), Mwamelo (St Francis), Rubuga (Marian), Mpanduji (Mazinde Juu), Lisa Chille (St Francis), Elizabeth Ng’imba (St Francis), Doris Noah (Kandoto, K’njaro), Herieth Machunda (St Francis) na Daisy Mugenyi (Kifungilo). Wavulana 10 bora ni Swai (Feza), Maugo (St Joseph Millennium), Tilubuzya (Thomas More Machrina), Mbangalukela (St Joseph Millennium), Rutatora (Feza), Simon Mnyele (Feza), Pascal Madukwa (Nyegezi Seminary), Henry Stanley (St Joseph Millennium), Fransisco Kibasa (Mzumbe) na Tumaini Charles (Ilboru).
Posted by MROKI On Wednesday, February 08, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo