Nafasi Ya Matangazo

February 03, 2012

Katika pita pita yangu katika mitaa na viunga vya Jijini Dar es salaam nilibahatika kukutana na muuza madafu huyu ambaye baiskeli yake kafunga mataa mengi ikiwapo tochi, taa za Pikipiki, gari na za baiskeli lakini katika hizo ambazo pia ziliendana na midoli na reflection za aina mbalimbali. 

Licha ya taa hizo kuwa nyingi lakini hakuna hata moja inayowaka kiasi cha mtu mmoja aliyekuwa akinywa madafu kwa jamaa huyo huko Mabwepande kudai kuwa Taa hizo ni sawa na zile za barabarani ambazo zipo nyingi jijini hapa lakini haziwaki akitolea mfano zuilizowekwa hivi karibuni barabara ya Mandela kuwa ziliwaka wiki moja tu.

Kwa wahusika hasa wakala wa barabara (TANROADS) hili ni dongo na kama sio ndogo basi hakikisheni taa hizo zinawaka zisiwe kama za huyu Mwenye hii baiskeli ambaye ameweka urembo.
Posted by MROKI On Friday, February 03, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo