Nafasi Ya Matangazo

November 25, 2011

Mchezaji wa Zanzibar Heroers Ali Badru akichuana na mchezaji wa Uganda Cranes Andrew Mwesigwa wakati timu hizo zikichuana katika mchezo wa kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii. 
 
Tayari mpira umekwisha ambapo Uganda Cranes imeifunga Zanzibar Heroers magoli 2-1 goli la kwanza la Uganda Cranes limefungwa na Mchezaji Danny Wagaruka katika kipindi cha kwanza, huku Mike Serumaga akifunga goli la pili katika kipindi cha pili, goli la kufutia machozi kwa upande wa Zanzibar Heroers limefungwa na mchezaji Ali Badru katika kipindi cha pili
Mashabiki mbalimbali wakishuhudia mpambano huo kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Mashabiki mbalimbali wakishuhudia mpambano huo kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Wadau mbalimbali wamekuwepo katika kushuhudia mpamabano huo kutoka kulia ni Adam Mgoyi, Evance Aveva, Bw. Mulamu, Said Tuli na Patrick Kahemele wakifuatilia mchezo huo.
Wadau kutoka Serengeti Breweries nao walikuwepo kwani wao ndiyo wawezeshaji au wadhamini wa mashindano haya mtari wa juu kutoka kulia ni Moses Keba, Mr. Ssebo, mstari wa chini kutoka kulia ni Ritah Mchaki na Maurice Njowoka
Aliyewahi kuwa kocha wa Yanga Sredojevic Milutin 'Micho' akishuhudia mchezo huo.
Kampteni wa Uganda Cranes Andrew Mwesigwa kushoto na Kapten wa timu ya Zanzibar Heroers Nadir Canavaro wakipata maelezo kutoka kwa marefa wa mpambano huo.
Kikosi cha Uganda Cranes katika picha.
Kikiso cha Zanzibar Heroers katika picha.
Wachezaji wa Zanzibar Heroers na Uganda Cranes wakisalimiana kabla ya mchezo huo kuanza leo jioni kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Posted by MROKI On Friday, November 25, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo