Makamu wa Rais Mohammed Gharib Bilal akinyanyua juu mshumaa kuashiria ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 10 ya Chama cha Umoja wa Wabunge la Bunge la Tanzania wa kupambana na Ukimwi (TAPAC) katika sherehe zilizofanyika leo katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma leo tarehe 18/11/2011.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya picha Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wa Tanzania wa kupambana na Ukimwi (TAPAC), Lediana Mng’ong’o, kwa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia umoja huo, wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umoja huo tangu ulipoanzishwa. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma leo Novemba 18, 2011. Kulia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda.
Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilal akimpa Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wa Bunge la Tanzania wa Kupambana na Ukimwi (TAPAC) Lediana Mng’ong’o (katikati) zawadi ya picha kuashiria ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 10 ya Umoja huko katika sherehe zilizofanyika leo tarehe 18/11/2011 katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal akimpongeza Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wa Bunge la Tanzania wa kupambana na ukimwi, Lediana Mng’ong’o kwa kuongoza Umoja huo katika kipindi cha miaka 10.
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal akiwasha mshumaa kuashiria ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 10 ya Chama cha Umoja wa Wabunge la Bunge la Tanzania wa kupambana na Ukimwi (TAPAC) katika sherehe zilizofanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa mjini Dodoma leo tarehe 18/11/2011.
0 comments:
Post a Comment