LOLOTE LAWEZEKANA CHINI YA JUA: NIMEFIKA KILELE CHA MLIMA
Jina langu ni Josephat Torner ni mwafrica niliyezaliwa na ulemavu wa ngozi
Nahisi kama maisha yangu yote nimekuwa nikipanda mlima mrefu. Nimepanda na nimepambana na unyanyapaa na ubaguzi wa kila siku. Nimepigania kuthaminiwa, nimeanguka lakini kila mara nimeinuka, nimepoteza kaka na dada zangu njiani.
Kwa muda wa siku 8 zilizopita nimetembea kwa ajili ya albino wote Africa ambao kwa namna fulani maishani mwao wamejisikia kama mimi. Nimetembea kwa ajili ya Ukombozi wetu
Kupanda mlima huu mrefu kuliko yote ni kazi ngumu kulikozote nilizowahi kufanya, vita ambayo nisingekubali kushindwa
Kwangu mimi,Leo nimefika kilele cha mlima, Pengine mimi ni mutu wa kwanza albino kufika kufika kilele kirefu kuliko vyote Africa , natazama pande zote za Bara letu nawaambia Waafrica wote na watu wote kuwa Albino ni binadamu anayejiweza kama wengine . Sote ni Waafrica kamwe si wanyama. Hadi kufikia leo yawezekana mumekuwa munaona mwafrica Albino. Natumaini leo hii munaona mutu
Nawaambia Albino wote Africa,tokeni gizani sasa na musiendelee kamwe kuishi kivulini mwa jua, Nimepambana na Mlima, nimepambana na Juan a sote sasa nafahamu twaweza kuwa huru
Tusimame sote kwa pamoja tupigane hii vita , kwani leo sote tunadai haki yetu ya kuishi.
0 comments:
Post a Comment