Nafasi Ya Matangazo

July 08, 2009

Mkuu wa Ulinzi wa bandari akizungumza na waandishi.
Wafanyakazi wa bandari wakiingia baada ya tukio la udanganyifu wa kuwapo kwa mabomu kwisha.
Leo asubuhi wafanyakzi wa bandari ya dar es Salaam walikubwa na kizaa zaa baada ya kutangaziwa kuwapo kwa boti katika bandari hiyo ambayo inamabomu.
Kufuatia amri hiyo wafanyakzi wote walio ndani ya bandari hiyo waliamriwa kutoka nje ya eneo hilo maana ilikuwa inatakiwa kulipuliwa iwapo jitihada za kuyategua mabomu hayo zingeshindaka.

Vikosi vya uoakojai vya Zimamoto, Polisi, JWTZ na Waandishi wa habari ni miongoni mwa wawajibikaji waliofika katika eneo la tukio hilo la uigizaji.

'Mabomu' yaliyokutwa katika boti hiyo yakiwa katika gari la polisi DFP 2724.

Pichani ni matukio kadhaa ya maigizo ambayo yalifanyika baada ya mabomu hayo ambayo yalikuwa ni Matikitiki maji, Matango, Biringanya kuwekwa sawa.

Kufuatia hatua hiyo waandishi wa habari wameonya udanganyifu mkubwa uliofanya na bandari hiyo na kuwa siku nyingine linaweza tokea tukio la kweli na taarifa zisiaminike.
Posted by MROKI On Wednesday, July 08, 2009 1 comment

1 comment:

  1. AnonymousJuly 11, 2009

    kwa wenzetu wa dunia iliyoendela hiyo ni sehemu ya maisha kila mwezi kuna mazoezi kama hayo mpaka mashuleni, sasa waandishi wa bongo waliosoma ambao hawajawahi kusafiri ng'ambo ya Mto Ruvu yaani taabu

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo