Nafasi Ya Matangazo

May 15, 2024











bababa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema sekta ya utalii ina mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa nchi kupitia  usafiri wa anga ambao ni kichochea kikuu cha ukuaji wa uchumi.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua Kongamano la sita la usafiri wa anga Jumuiya ya  Afrika Mashariki katika Hoteli ya Verde Mtoni, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 15 Mei 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza hatua iliyofikiwa na SMZ  katika ukuaji wa sekta ya usafiri wa anga  ya kutekeleza miradi  kwa  kukamilisha jengo la abiria uwanja wa ndege wa  Kimataifa  wa Abeid Aman Karume Terminal 3, kuanza ujenzi jengo jipya la abiria Terminal 2 litakalohudumia abiria zaidi 1,300,000 kwa mwaka, ujenzi na ukarabati wa ujenzi wa jengo la zamani la Terminal 1, ujenzi wa jengo la biashara na ofisi katika jengo la tatu la abiria, jengo la kuhifadhi na kusafirisha hasa chakula vinavyoharibika kwa haraka,  ujenzi wa vituo vitatu vya huduma za mafuta ya ndege, ujenzi wa uwanja wa ndege na upanuzi wa kiwanja cha ndege Pemba na jengo jipya la abiria na uwanja wa ujenzi wa kiwanja cha Nungwi.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewahimiza washiriki  wote wa kongamano hilo kujadili na kutoa mapendekezo kwa kubainisha fursa zitazoweza kutumika katika sekta ya usafiri wa anga kwa manufaa ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Mashariki .
Posted by MROKI On Wednesday, May 15, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo