Nafasi Ya Matangazo

June 05, 2023


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanya operesheni kwa siku mbili mfululizo wilaya ya Arumeru katika vijiji vya Kisimiri juu na Lesinoni na kukamata jumla ya gunia 731 za bangi kavu pamoja na kuteketeza hekari 308 za mashamba ya bangi.

Katika Kijiji cha Kisimiri juu, Mamlaka ilikamata gunia 482 za na kuteketeza jumla ya hekari 101 za mashamba ya bangi na kijiji cha Lesinoni yalikamatwa magunia 249 za bangi kavu na kuteketeza hekari 207 ambapo jumla ya watuhumiwa 9 wamekamatwa kuhusiana na dawa hizo.

Ukamataji huo umefanyika tarehe 31 mwezi Mei na tarehe 01 Juni, 2023 kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kufanya operesheni nchi nzima ili kuhakikisha dawa za kulevya zinatokomezwa nchini. Operesheni hizi zimefanyika siku moja baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) kutoa taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya nchini kwa mwaka 2022 ambayo iliitaja mikoa ya Arusha, Iringa, Morogoro na Manyara kujihusisha na kilimo cha bangi kwa kiasi kikubwa.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya  kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama itaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara katika maeneo yote nchini ili kuhakikisha kilimo cha bangi na mirungi kinatokomezwa kabisa na wananchi kujikita katika kilimo cha mazao mbadala ya biashara na chakula.
 
Aretas Lyimo
Kamishna Jenerali
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya
Posted by MROKI On Monday, June 05, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo