Nafasi Ya Matangazo

February 19, 2015


Mwakilishi wa jimbo la Magomeni, Salmin Awadhi Salmin (pichani) amefariki dunia ghafla mchana huu akiwa mkutanoni katika ofisi kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar.

Salmin Awadh ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM  na Mnadhimu wa wajumbe wa CCM Baraza la Wawakilishi Zanzibar amefariki wakati akihudhuria vikao vya chama.

Marehemu Awadh alikimbizwa kwa matibabu Hospitali ya Mnazi Mmoja, Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa uchunguzi zaidi. 

Aidha taarifa kutoka ofisi Katibu wa Baraza la wawakilishi, iliyotolewa kwa waandishi wa habari kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Utawala, Amour Mohamed Amour imesemwa mwili wa marehemu utaagwa kesho saa 5 asubhi katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi na baade katika maziko yatakayo fanyika makunduchi.
Father Kidevu Blog inatoa pole kwa Wana Magomeni, Familia ya Marehemu, Ndugu jamaa na Marafiki wote na Wazanzibar wote kufuatia msiba huo.
Posted by MROKI On Thursday, February 19, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo