Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amempongeza Miss Grand International Tanzania 2026 Jihan Dimack kwa kutwaa taji la Dunia la mashindano hayo.
Rais Samia amesema katika pongezi hizo alizozichapisha katika ukurasa wake wa Instagram kua Jihan ameipeperusha vyema bendera ya Tanzania.
"Ninakupongeza kwa dhati mwanangu, Jihan Dimack, kwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania na kutwaa taji la Miss Grand International 2026," alisema Rais Samia.
Rais amesema ushindi huo ni fahari kwa taifa nankielelezo cha uwezo wa Watanzania kufikia mafanikio.
"Ushindi huu ni fahari kwa Taifa letu na kielelezo cha uwezo wa Watanzania kufikia mafanikio makubwa tunapoungana na kushirikiana. Pia, ni chachu kwa vijana, hususan wasichana, kujiamini, kuthubutu na kusimamia ndoto na vipaji vyao," aliongeza Rais Samia.
Rais Samia alimalizia ujumbe wake huo kwa kusema "Hongera sana. Ninakutakia kila la kheri".
Jihan ametwaa taji hilo na kuwashijda warembo kutoka nchi mbalimbali huku akiwa ni Mtanzania wa kwanza kutwaa taji hilo tangu lianzishwe mwaka 2013.









0 comments:
Post a Comment