Nafasi Ya Matangazo

October 09, 2026







Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb) amewataka wazalishaji wa saruji nchini kuhakikisha wanaepuka tabia ya kuhujumu soko kwa kufanya mjengeko wa bei za saruji kwenye soko.

Amesema hayo mkoani Mbeya wakati wa ziara yake katika Kiwanda cha Saruji cha Mbeya Cement ambapo alikagua shughuli za uzalishaji, kusikiliza changamoto zao na kutambua fursa zilizopo katika sekta ya viwanda.

Waziri Kapinga amesema serikali iko makini na itachukua hatua stahiki kwa wazalishaji au kiwanda cha saruji kitakapobainika.

Vilevile amewataka kuhakikisha wanazalisha saruji kwa wingi na kuwafikia wananchi wa chini kwa bei iliyopangwa kwa kupitia mawakala wao.

Aidha Waziri Kapinga pia ametembelea  Kiwanda cha Magodoro cha G&B na Kiwanda cha TBL ambapo amesisitiza kuwa Serikali haitakubali changamoto za wafanyabiashara kubaki bila majibu, hivyo ziara katika maeneo ya uzalishaji zitaendelea kutumika kama sehemu ya kusikiliza kero, kutambua fursa na kuweka mikakati ya kuzitatua.
Posted by MROKI On Friday, October 09, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo