Na Mwandishi wetu, Kigoma
MKUU wa Wilaya ya Buhigwe, Mkoani Kigoma, Col Marco Gaguti
(pichani juu) ameeleza kutoridhishwa kwake na kasi ya Ukusanyaji mapato na uibuaji wa vyanzo
vipya vya mapato wilayani Buhigwe.
Kanali Gaguti alisema hayo baada ya Halmashauri
hiyo kushindwa kufikia lengo la ukusanyaji wa mapato ya ndani ya
takribani shilingi milioni 600 yaliyokusudiwa kukusanywa na badala yake
kukusanya asilimia 41 tu kwa mwaka wa fedha wa 2015/16 licha ya kuwa na
vyanzo vingi vya mapato vilivyopo katika Halmashauri hiyo.
Aliwataka madiwani kwa kushirikiana na watendaji
kuibua vyanzo vipya vya mapato ili kuvuka lengo hilo kwa mwaka huu wa 2016/17.
Kanali Gaguti aliyasema hayo jana katika kikao cha
baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo wakati wakijadili Malengo ya ukusanyaji
wa mapato kwa kipindi cha mwaka 2016/17 iliyo wasilishwa katika kikao hicho
ikiwa na lengo la kukusanya kiasi cha shilingi milioni 600 na kujadili kwanini
halmashauri hiyo ilishindwa kufikia malengo ya mwaka wa fedha 2015/16.
Gaguti alisema hayupo tayari kuona halmashauri
hiyo inakusanya mapato chini ya kiwango kwasababu za uzembe wa kubuni
mbinu za ukusanyaji wa mapato kwa halmashauri iliyo mpakani na nchi
jirani ya Burundi haiwezi kukusanya sh milioni 600 ni ndogo Sana waongeze
ifikie hata bilioni moja.
Aliwataka madiwani washirikiane na
Watendaji kuibua vyanzo vipya vya mapato na kuweka mikakatii na muda
wa kukamilisha mikakati hiyo ili kuhakikisha Halmashauri hiyo inafikia malengo
ya ukusanyaji mapato kwa mwaka 2016/17 kuepukana na changamoto ya halmashauri
hiyo kukosa fedha za kuiendesha.
“Ningependa
tuanze kuainisha makosa na uzembe tulio ufanya katika ukusanyaji wa
mapato ya ndani uliyo pelekea ukosefu wa fedha za
halmashauri na tuandae mkakati wa kukabiliana na uzembe huo ambao
hauvumiliki. Serikali ya Wilaya itasimama imara kushirikiana na wadau wote
kuhakikisha lengo linafikiwa kwa wakati," alisema Kanali Gaguti.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Buhigwe, Elisha Bagwenya alisema Baraza lake linaunga mkono hoja ya
Mkuu wa wilaya na kusema kuwa Halmashauri inavyanzo vingi vya mapato hivyo uandaliwe
utaratibu wa Mkurugenzi na watendaji na madiwani kuunda kamati itakayo kwenda
kusimamia mapato ya halmashauri yanayo potea bila sababu kutokana na vyanzo
vingi kuwa chini ya usimamizi wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA na Askari wa
mipakani.
Alisema Halmashauri iunde vyanzo vipya vya mapato
ikiwa ni pamoja na kuuza vibanda na viwanja kwa wafanya biashara wa Mnanira,
Nyamugali, Kilelema na Muyama ambako kuna masoko ya ujirani mwema,
na kujenga kituo cha magari Manyovu vyanzo hivyo vita saidia kuongeza
mapato ya Halmashauri.
Aidha alimuomba Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo kuurudisha mnada wa Ng’ombe katika kijiji cha
Buhigwe ili wafugaji kutoka Burundi na Tanzania Waweze kuja kuuza na kununua
Ng’ombe na mbuzi katika mnada huo na Halmashauri iweze kuingiza mapato kupitia
mnada huo.
Nae Diwani wa kata ya Janda Pasco
Nkeyemba alisema tatizo linalo pelekea Halmashauri kushindwa
kukusanya mapato ni uzembe wa watendaji Kwani kuna baadhi ya masoko hayana
madaftari ya kukusanyia mapato katika masoko na watu wanaingia sokoni kufanya
biashara bila kulipia ushuru wa Halmashauri.
0 comments:
Post a Comment