Nafasi Ya Matangazo

September 16, 2016



 Mkuu wa Wi;laya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Kanali Marco Gaguti.
 Na Mwandishi wetu, Kigoma
MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Col Marco Gaguti amewaonya watendaji wa Wilaya ya Buhigwe kuepuka kuwa chanzo cha migogoro ya Wananchi kwa kukwamisha shughuli za maendeleo ya Wananchi  na kulinda maslahi yao binafsi na kushindwa kuwatumikia Wananchi ipasavyo.

Wito huo aliutoa jana katika Mkutano wa hadhara  uliofanika katika viwanja vya shule ya  msingi Buhigwe wakati akipokea malalamiko ya Wa nanchi wa vijiji vya Buhigwe na mlela aliwaomba watendaji kutatua kero hizona kuacha tabia ya kuchochea migogoro ya Wananchi.

Gaguti aliwataka Watendaji kuwahudumia Wananchi kwa haraka na kutatua kero mbalimbali zinazo wakabili ili kupunguza migogoro na kuepuka kua chanzo cha migogoro kwa Wananchi kwakuwa serikali ya awamu ya tano ni serikali inayo wahudumia wananchi na sio Serikali inayo jail maslahi ya mtu binafsi.

“kiongozi ambaye amekuwa chanzo cha  migogoro  badala ya kuwa njia ya kutatia migogoro hiyo  na kiongozi ambaye hashughulikii matatizo ya Wananchi kwa wakati  hatufai  wale ambao wapo chini ya mamlaka yangu tukiwabaini  tutawachukulia hatua za kisheria, na kwa wale mlio wachagua na hawaendani na  na malengo mlio jiwekea watoeni taratibu zipo wazi”,alisema Mkuu  wa Wilaya. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


Hata hivyo katika mkutano huo Gaguti aliwaomba Wananchi kuendelea kudumisha amani kwa kushirikiana na vyombo vya dola katika kuwabaini  watu wenye nia mbaya na wahamiaji haramuambao baadhi yao wamekuwa chanzo cha uhalifu.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buhigwe Venas Kigwinya  alisema kumekuwa na malala miko mengi kutoka kwa Wananchi kutoka katika kijiji cha mlela waki mtuhumu mendaji wa kijiji katika suala la maji kuwa fedha zinazo kusanywa kwenye vyanzo vya maji hazijulikani zina kwenda wapi  na kwenye mikutano ya kijiji Wananchi hawasomewi mapato na matumizi yatokanayo na makusanyo ya fedha za maji.

Kigwinya alisema eneo linguine la migogoro inyo sababishwa na watendaji ni suala la uuzaji wa viwanja bila kufuata utaratibu na wa uuzaji wa viwanja hivyo, na suala lingine ni uuzaji wa misitu ya kijiji kwa kutoa taarifa za uongo na kero hizo alizitatulia ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kwenda kumomba Mkurugenzi kumuondoa mtendaji huyo na kuwaletea Mtendaji anae jali maslahi ya Wananchi.

 Kwa upande wao Wananchi wa Kijiji cha Mlela ,Festo Nyamunda na Rejina Laurenti walisema kumekuwa na kero ya  viwanja kuuzwa na mtendaji na Mwenyekiti wa Kijiji bila kufuata utaratibu wa kuwashilikisha Wananchi suala linalo pelekea migogoro kwa Wananchi, mpaka sasa katika kijiji hicho hakuna maeneo yaliyo tengwa  kwaajili ya huduma za kijamii kama Shule na vtuo vya Afya ili kuwasaidia Wananchi hao.

Walisema kunatatizo lilijitokeza katika Kijiji hicho cha Mwenyekiti wa kijiji na Mtendaji waliuza msitu miti 200 na kuwadanganya Wananchi miti iliyo uzwa ni miti 15, na sisi tunaona miti inaendelea kukatwa hiyo ni moja ya sababu inayo weza kupelekea migogoro baina yetu wana kijiji na wawekezaji inayo sababishwa na watendaji hao.
Posted by MROKI On Friday, September 16, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo