Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi
WATU 13 wamepoteza maisha na
wengine 11 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyoyahusisha magarui mawili
ya abiria kugongana katika eneo la Mwamaya Wilayani Kwimba mkoani Mwanza leo
asubuhi.
Akizungumza na Habarileo online, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo tukio
na kusema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya Saa 12:15 asubuhi na ilihusisha
gari dogo la abiria Toyota Hiace lenye namba za usajili T368 CWQ lililokuwa
likotokea kijiji cha Shirima kwenda Mwanza mjini na kugonagana na Basi aina ya
Scania lenye namba za usajili T874 CWE.
Kamanda Msangi alisema kuwa ajali hiyo
ilitokea wakati gari hilo dogo likiingia katika barabara kubwa na kugongana na
basi hilo lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Mwanza na kusababisha vifo hivyo
kwa abiria na majeruhi waliokuwa katika gari hilo dogo.
“Nipo njiani naenda eneo la
tukio lakini taarifa za awali nilizopokea ni kuwa watu 13 wamefariki duniani na
wengine 11 wamejeruhiwa na kati ya hao marehemu wawili ni watoto wadogo, na
ajali imetokea katika makutano ya barabara kuu na hiyo ya kutokea kijiji cha
Shirima ili pokuwa ikitokea gari ndogo.SOURCE: Habarileo Online.
0 comments:
Post a Comment