Nafasi Ya Matangazo

September 10, 2009

Lori la mizigo mali ya KLM Trasport lenye namba za usajili T934 ASM likiwa limeparamia nyumba na kuua mtu mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Ndete mkazi wa Kimara Mwisho Dar es Salaam.

Lori hili lilikuwa limeegeshwa kando kando ya barabara na kuparamia nyumba hiyo majira ya saa kumi alfajiri na kumuua mtu huyo aliyerkuwa amelala kabla ya kutaka kugonga nyumba nyingine.


Mke wa Marehemu na mtoto wao walikuwa wamekwenda msibani hivyo baba kubaki pekeyake katika nyumba hiyo ya vymba viwili na sebule.

Kijana mwingine ambaye ni kondakta wa daladala maarufu kwa jina la "Chinga" alijeruhiwa
Lori hilo likiwa limekwama kabla ya kuparamia nyumba nyingine.Wakzi wa Kimara Mwisho wakiangalia ajali hiyo.Polisi Usalama Barabarani wakiwa katika tukio hilo.
Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa ni zaidi ya magari 5 yamesha kosa kosa kuparamia nyumba za eneo hilo na yote yanakuwa yameegesha na madereva wake kwenda kupumzika.


Mini Busshiyo iliyokuwa im,eharibika na kusubiri matengenezo imeharibiwa vibaya na malori hayo kiasi cha kuonekana kuwa iliwahi pinduka.
Posted by MROKI On Thursday, September 10, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo