Nafasi Ya Matangazo

March 25, 2024

 









Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde leo Machi 25, 2024  amefika katika eneo la Malera Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara kwa ajili ya utatuzi wa mgogoro baina ya wachimbaji wadogo wamiliki wa Leseni na Kampuni ya KIRIBO ambao ulipelekea zuio la mgawo wa mawe mpaka baada ya utatuzi wa mgogoro huo.

Waziri Mavunde ametumia takribani saa 6 kutatua mgogoro husika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, watendaji wa wizara na viongozi wa wachimbaji wadogo mkoa wa Mara (MAREMA)

“Ni maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya utatuzi wa migogoro mbalimbali katika sekta hii ya madini ambayo inadhoofisha kukua kwa uzalishaji wa madini," amesema Mavunde 

Aidha, amezipongeza  pande zote kwa kuridhia makubaliano katika hatua ya awali ya kutatua mgogoro huo.

Ameongeza kwamba kwa kuwa kulikuwa na zuio kwamba mgao wa mawe yaliyozalishwa usimame kwasababu ya mgogoro huu, ameelekeza  zuio hilo liondolewe na mgao wa mawe uanze kesho mapema tarehe 26.03.2024.

"Pia, hakikisheni katika utekelezaji wa wa maridhiano haya,  wachimbaji wadogo hawaondolewi katika eneo hilo na waachwe waendelee na shughuli zao," amesema Mavunde.

Akitoa maelezo ya awali, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mtanda amemshukuru Waziri Mavunde kwa kufanikisha utatuzi wa mgogoro husika na kupongeza hatua za kuruhusu mgao wa mawe kwa kuwa hali ya kipato ya wananchi wa eneo hilo ilikwenda chini na mapato ya serikali kutopatikana kwa wakati.

Zaidi ya watu 2000 wananufaika na mgodi huo ambao umekuwa ni shughuli kubwa ya kiuchumi ya wananchi wa Malera.
Posted by MROKI On Monday, March 25, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo