Nafasi Ya Matangazo

March 25, 2024

Mwanzilishi wa maktaba ya kijamii wilayani Mwanga, Jennifer Dickson akifurahia tuzo ya Malkia wa Nguvu ajaye katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
****************
Nyota ya Mwanafunzi wa Kike wa kitanzania Jennifer Dickson na mwanzilishi wa maktaba ya kijamii wilayani Mwanga anayesoma elimu ya Chuo Kikuu mwaka wa pili nchini Rwanda katika Chuo cha Global Health Equity, akisomea fani ya Udaktari, inazidi kung’aa ambapo ametunukiwa tuzo ya Malkia wa Nguvu Ajaye 2024 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Tuzo hizo hutolewa na Clouds Media Group.

Maktaba aliyoianzisha Jennifer, inayojulikana kama maktaba ya kijamii ya Martha Onesmo, ilizinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwaka huu ipo katika kata ya Msangeni kwa ajili ya kuwahudumia watu wote. Mgeni rasmi katika uzinduzi wake alikuwa ni Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda.

Akiongea muda mfupi baada ya kupokea tuzo hiyo, alisema kuwa amefarijika kwa kiasi kikubwa kuona mchango wake katika jamii umetambuliwa na tuzo hiyo imezidi kumtia moyo wa kuendelea kufanya kazi za kijamii zenye mwelekeo wa kunufaisha watu wengi.

Alitoa shukrani kwa wazazi wake,marafiki zake na wa familia,na wafadhili mbalimbali ambao wamemsaidia kufanikisha ndoto yake ya kufungua maktaba ya kijamii ambayo imepelekea apate tuzo ya Malkia wa Nguvu ajae inayotolewa na kampuni ya habari ya Clouds.

Pia alitoa shukrani wa waandaaji wa tuzo hizo kwa kuona mchango wake katika jamii pia alitoa ushauri kwa vijana wenzake hususani watoto wa kike kujiamini na kupambana ili kufanikisha ndoto zao katika maisha na kuhakikisha hawabaki nyuma.

Kwa upande wa wazazi wake, walisema wamefurahi kuona kijana wao anapata mafaniko “Tuzo hii ni kielelezo kikubwa kwamba mtoto wa kike anaweza kama akiwezeshwa. Jennifer ni matokeo ya juhudi zake na ushirikiano wa jamii nzima inayomzunguka ukiaanza na sisi wazazi wake, ndugu zake wengine wa karibu hasa bibi yake mama Cecilia Ezekiel na jamii nzima ambayo ilishirikiana naye kwa hali na mali kuhakikisha anatimiza ndoto yake. Ni watu wengi wanamchango wao wa hali na mali katika kufikia hapa tulipo leo” Alisema Dk. Linda Ezekiel.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya maktaba hiyo, Profesa Bonaventure Rutinwa, ambaye pia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amempongeza Jennifer kwa kufikia mafanikio hayo,”Ni jambo la kufurahisha kuona kijana wa umri wake anakuwa na ubunifu wa mradi ambao unaleta athari chanya kwa jamii hususani katika maeneo ya vijijini ,natoa wito kwake aendelee kupambana ili aweze kufanya mambo makubwa kwa jamii na taifa kwa ujumla”. Alisisitiza.

Wakati wa uzinduzi wa maktaba hiyo ya kijamii ya Martha Onesmo, mwanzilishi wake Jennifer alisema ndoto ya kuanzisha maktaba hiyo alikuwa nayo yangu anasoma kidato cha sita kwa ajili ya kuwezesha wakazi wa vijijini kupata maarifa.
Picha ya pamoja ya wanafamilia ya Jennifer na marafiki wa familia.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji) Dk. Kitila Mkumbo (kulia) akimpongeza mshindi wa tuzo la Malkia wa Nguvu ajaye,Jennifer Dickson katika hafla ya kutunuku tuzo hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam,katikati ni mwenyekiti wa bodi ya maktaba ya kijamii ya Mwanga iliyoanzishwa Jennifer, Profesa Bonaventure Rutinwa, ambaye pia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wanafamilia ya Jennifer na mwenyekiti wa maktaba ya Martha Onesmo wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.
Jennifer akiwa na wazazi wake.
Jennifer akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya maktaba ya Martha Onesmo,Profesa Bonaventure Rutinwa.
Posted by MROKI On Monday, March 25, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo