Nafasi Ya Matangazo

March 15, 2024

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. 
Ephraim Mafuru.
*********
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na utenguzi wa viongozi kama ifutatavyo: 
Amemteua Bw. Ally Senga Gugu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Gugu alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma.
Amemteua Bw. Kaspar Kaspar Mmuya kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma. Kabla ya uteuzi huu Bw. Mmuya alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Amemteua Mhandisi Mwajuma Waziri kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji. Kabla ya uteuzi huu Mhandisi Waziri alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji.

Mhandisi Waziri anachukua nafasi ya Prof. Jamal Katundu ambaye uteuzi wake umetenguliwa. 

Amemteua Bw. Ephraim Mafuru kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Kabla ya uteuzi huu Bw. Mafuru alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). 

Bw. Mafuru anachukua nafasi ya Bw. Damasi Mfugale ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Ametengua uteuzi wa Bw. Richard Rwanyakaato Kiiza, Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA).

Posted by MROKI On Friday, March 15, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo