Nafasi Ya Matangazo

March 15, 2024

Na Mwandishi wetu, Iringa
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor H. Seff ameongoza Kamati ya Utendaji ya Mradi wa RISE Machi 14, 2024 kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za Wenda-Mgama (19km) na Mtili-Ifwagi-Mkuta (14km) kwa kiwango cha lami.

Ujenzi huo unatekelezwa na Mkandarasi CHICO katika Halmashauri za Wilaya ya Iringa na Mufindi.

Msimamizi Mshauri wa Mkandarasi  Afrisa ameeleza maendeleo ya mradi yapo chini kutokana Mkandarasi kutokukamilisha idadi ya  Mitambo na Watumishi katika eneo la Kazi. 

Hata hivyo, Mkandarasi CHICO ameahidi kumaliza kazi kwa muda uliowekwa kwenye mkataba. 

Mhandisi Seff amemtaka Mkandarasi CHICO kuongeza kasi ya ujenzi ili kufidia muda uliopotea na ifikapo mwezi juni mwaka 2024 kama atashindwa kufikia malengo yaliyowekwa kwa mujibu wa mkataba hatasita  kuvunja Mkataba.

Miradi yote miwili inatarajiwa kukamilika hadi kufikia mwezi februari, 2025.

Mradi wa RISE unalenga kuboresha barabara zenye fursa za kiuchumi hasa maeneo yenye uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa kujenga barabara za lami.

Pia, kufanya matengenezo na kuboresha  maeneo Korofi (bottleneck) ya mtandao wa barabara za Wilaya ili kukuza uchumi na kuongeza fursa za ajira. 

Mradi wa RISE unatekelezwa na TARURA kwa kipindi cha miaka sita kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2026/2027.
Posted by MROKI On Friday, March 15, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo