Nafasi Ya Matangazo

April 28, 2024




Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Leo Aprili 28, 2024 ameshiriki Ibada Maalumu ya uwekeji wa Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) la Mtaa wa Area A Kata ya Chamwino Jijini Dodoma.

Ibada hiyo maalumu iliongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Steven Mulenga ambapo tukio hilo limekwenda sambamba na Uzinduzi wa  Mtaala wa kufundishia vijana na watoto kwenye Makanisani hayo.

Mhe. Senyamule ametoa salaam kwa waumini waliohudhuria ibada hiyo na  kuwajulisha juu ya fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya Mkoa wa Dodoma. 

Pia aliwakumbusha kazi nzuri inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ibada hiyo iliongozwa na neno lisemalo “Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko ule wa kwanza, asema Bwana wa majeshi” Hagai 2:9.
Posted by MROKI On Sunday, April 28, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo