Nafasi Ya Matangazo

September 28, 2021

Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bi.Hasina Omari.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa wajumbe watatu (3) kujaza nafasi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Wajumbe walioteuliwa na Rais kwa mujibu wa Sheria ni Bi Asina Abdillah Omari (pichani juu) aliteuliwa kwa kipindi cha pili kuendelea na majukumu ya Tume, baada ya kipindi chake cha kwanza kumalizika tarehe 15 Septemba, 2021. 

Pia amemteua  Mhe. Magdalena Kamugisha Rwebangira, kutoka Chama cha Wanasheria (TLS). 

Aidha Rais Samia amemteua  Mhe. Jaji Jacob Mwambengele, Jaji wa Mahakama ya Rufani. Uteuzi huu umeanza tarehe 14 Septemba, 2021.
Posted by MROKI On Tuesday, September 28, 2021 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo