Nafasi Ya Matangazo

September 28, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Ufaranza Nchini Mhe. Nabil Hajlaoui, muda mfupi baada ya Balozi Nabil kukabidhi Hati ya Utambulisho Ikulu Chamwino Jijji Dodoma leo Sept 27,2021. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Somalia Nchini Mhe. Zahra Ali Hassan, muda mfupi baada ya Balozi Zahra kukabidhi Hati ya Utambulisho Ikulu Chamwino Jijji Dodoma leo Sept 27,2021. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 27 Agosti, 2021
amepokea Hati za Utambulisho wa Mabalozi wawili walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha Hati za Utambulisho ni Mhe. Zahra Ali Hassan Balozi wa  Somali na Mhe. Nabil Hajlaoui Balozi wa Ufaransa wote wakiwa na makazi yao hapa nchini.

Akizungumza mara baada ya kupokea hati hizo, Mhe. Rais Samia amewapongeza Mabalozi hao na kuwaomba kufikisha salamu zake kwa viongozi wakuu wa nchi zao na kusisitiza kuwa Tanzania itaendeleza uhusiano na ushirikiano kwa manufaa ya pande zote.

Kwa upande wao Mabalozi hao wamempongeza Mhe. Rais Samia kwa utendaji mzuri na kumuahidi ushirikiano.

Mabalozi hao wameeleza kuwa mataifa yao yana dhamira ya dhati ya kuimarisha uhusiano katika sekta mbalimbali hususan biashara na uwekezaji.

Wakati huohuo, Mhe. Rais Samia amemuapisha Mhe. Balozi Togolani Edriss Mavura kuwa Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini.

Pia, Mhe. Rais Samia amemuapisha Bw. Mathew Modest Kilama kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma.

Hafla hiyo ya uapisho ilioyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Posted by MROKI On Tuesday, September 28, 2021 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo