Nafasi Ya Matangazo

November 13, 2016

Baada ya watanzania kushuhudia Jua kupatwa Kipete Septemba 1 mwaka huu kule Wanging'ombe Mkoani Njombe na Rujewa Mkoani Mbeya ikiwa ni tukio la kihistoria kupata kutokea kwa vizazi vya sasa leo dunia tena na watanzania watapata fursa ya kipekee kushuhudia Mwezi mpevu.
Mwezi huu Mpevu utakaoonekana leo Novemba 14, siyo tu ni mwezi mpevu ulio karibu zaidi na Dunia mwaka huu, bali pia ni mwezi mpevu ulio karibu zaidi katika karne hii ya 21.
Hali ya mwezi mpevu kukaribia zaidi na dunia katika kipindi cha mwaka wowote ndicho kinajulikana kama Mwezi Mpevu Ajabu (Super Moon) na hii kwa sababu unaonekana mkubwa zaidi kuliko ule unaoonekana unapokuwa mbali zaidi kutoka duniani.
Kwa jina la kitaalamu Mwezi Mpevu Ajabu huitwa pia Perigee-syzygy. Kila mwaka kuna Mwezi Mpevu Ajabu, lakini huu wa leo ni wa ajabu kwa sababu ni wa karibu zaidi katika miaka 67 iliyopita tangu mwaka 1948, na hautakuwa karibu kiasi hiki tena kwa miaka 18 ijayo hadi Novemba 25, 2034.
Posted by MROKI On Sunday, November 13, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo