Nafasi Ya Matangazo

November 14, 2016

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye akimkabidhi Bendera ya Taifa Bi. Julietha Kabete(kushoto) Mrembo atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini Nigeria.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye akimkabidhi Bendera ya Taifa Julietha Kabete (kushoto) Mrembo atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini Nigeria.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa mrembo Julietha Kabete atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini Nigeria.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania. Kutoka Kulia ni Mkuu wa Itifaki, Albert Makoye, Katibu wa Kamati, Bosco Majaliwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Internationa Agency, Hasim Lundenga.
 ************
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye  ameahidi  kuendelea kufanya mageuzi makubwa katika mashindano ya urembo hapa nchini ili kuondoa dosari zinazojitokeza katika mashindano hayo.

Nape ametoa ahadi hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati akimkabidhi Bendera Mshiriki wa  Tanzania katika mashindano ya urembo Bara la Afrika kwa mwaka 2016 yatakayofanyika Novemba 28 mwaka huu nchini Nigeria.

Nnauye  ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa mashindano kama haya yanakuwa na tija kwa Taifa hasa katika kuleta ajira kwa vijana pamoja na kuitangaza nchi kimataifa kupitia urembo.

“Serikali  nia yake ni kuhakikisha kuwa jambo hili linakuwa bora, linaminiwa na kuheshimika hivyo  watanzania wote watajivunia uwepo wa mashindano ya urembo nchini” alisistiza Mhe Nnauye.

Aidha Mwakilishi wa Millen Magese group Ltd,Matukio Aranyande Chuma amesema kuwa shindano hili litailetea sifa Tanzania na ni kwa mara ya kwanza kufanyika hivyo wataitumia fursa hiyo kuitangaza nchi kimataifa kupitia urembo.

“ kwa niaba ya Millen Magese group Ltd tunatoa shukrani zetu kwa Serikali na Kamati ya Miss Tanzania kwa kutuunga mkono katika jambo hili na tunaahidi kufanya vizuri katika mashindano haya”Alisema  Chuma.

Kwa upande wake Mshiriki kutoka Tanzania anayekwenda kushiriki mashindano hayo Bi. Julietha Kabete ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuunga mkono mashindano mbalimbali ya urembo Tanzania inaposhiriki.

“Naahidi kuitangaza nchi yangu vizuri katika mashindano haya na naomba watanzania waniombee na wanipigie kura ili niweze kushinda na kuitangaza Tanzania kimataifa katika urembo” Alisema  Julietha.

Mashindano ya Miss Afrika yameanzishwa mwaka 2016 na Prof. Bena Yage ambaye ni Gavana wa Jimbo la Cross River nchini Nigeria kwa lengo kupata mabalozi wa nchi za Afrika watakaosaidia kutangaza na kuelimsha waafrika kuhusu uchumi unaozingatia utunzaji wa mazingira.
Posted by MROKI On Monday, November 14, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo