Nafasi Ya Matangazo

March 11, 2015


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata mapokezi makubwa mara baada ya kuwasili katika wilaya ya Bahi.
Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kujenga na kukiimarisha Chama mkoani Dodoma pamoja na kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilayni ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa akihutubia wananchi wa kijiji cha Nguji kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kusalimia na kushiriki uchimbaji mitaro ya kutandikia ma bomba.
 Wananchi wa kijiji cha Nguji wakiwasikiliza viongozi wao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto), Mkuu wa mkoa wa Dodoma Chiku Galawa wakishirikiana na wananchi wengine kuchimba mfereji wa kupitishia bomba la maji katika kijiji cha Nguji wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi nje ya ofisi ya CCM wilaya ya Bahi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mfumo wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya jua unaotumika kuvuta maji kutoka kwenye kisima kuelekea kwenye mashamba ya zabibu ya LUBALA Saccoss inayounganisha jumla ya vijiji vitatu ambavyo ni Lukali,Bankolo na Lamaiti.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wakijiji cha Lamaiti.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akielekea shambani kushiriki kuandaa shamba la zabibu katika kijiji cha Lamaiti, wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipata mapokezi makubwa katika kata ya Makanda kijiji cha Chonde wilaya ya Bahi mkoa wa Dodoma.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimia wananchi wa kijiji cha Chonde wilaya ya Bahi,mkoani Dodoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Chonde wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisimikwa kuwa Mzee wa heshima wa kijiji cha Chonde.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasha trekta kama ishara ya kuzindua mradi wa matrekta 19 ya wakulima waliojiunga kwenye vikundi katiaka kata ya Makanda.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma bango la wananchi wa kijiji cha Msisi ambao shule ya Msingi kwa Msisi iliondolewa paa na upepo mkali mwaka 2011 na haijaezekwa mpaka sasa mwaka 2015.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Msisi ambao shule yao imeezuliwa paa tangia mwaka 2011.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka katika eneo la shule ya msingi Msisi baada ya kukamilisha zoezi la kuichangia shule hiyo na itaanza kurekebishwa baada ya wiki mbili.
 PICHA ZAIDI
Posted by MROKI On Wednesday, March 11, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo