Nafasi Ya Matangazo

September 10, 2014

Zahoro Pazi wa Simba, akikimbia na mpira huku akifuatwa na Dereck Waluliya wa timu ya URA ya Uganda wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati ya timu hizo, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam July 20 2013 ambapo Simba ilala kwa mabao 2-1.
********
Wekundu wa Msimbazi Simba Sc ya jijini Dar e Salaam inataraji kushuka katika dimba la uwanja wa Taifa Ijumaa hii kuwava watoza ushuru wa Uganda URA katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Akizungumza na Father Kidevu Blog usiku huu, Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba, godfrey Nyange kaburu amesema mchezo huo utapigwa uwanja wa taifa ijumaa hii jioni na alfajiri ya jumamosi Simba watakwea pipa kwenda kuipamba siku ya Ndanda day mjini Mtwara.

Simba itashuka dimbani ikiwa na kumbuklumbu ya kufungwa goli 2-1 katika uwanja huo huo wakati wa mchezo wa kirafiki na URA.

 
Posted by MROKI On Wednesday, September 10, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo