Nafasi Ya Matangazo

September 10, 2014

 WATU wawili wamekufa papo hapo na saba wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Mnolela Manispaa ya Lindi ikihusisha gari la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Ajali hiyo ilitokea katika Barabara ya Mingoyo, baada ya kifaru cha jeshi  kugonga nyumba na kusababisha kifo cha Somoe Kamteule aliyekuwapo ndani. Pia askari mwenye namba Mt 10728 Pascal Komba alikufa katika ajali hiyo.

Gari hilo ni la Kikosi Namba 83, ambalo liliacha njia na kugonga nyumba mbili  na raia na kusababisha vifo hivyo. Dereva wa gari hilo alikuwa askari Shandili Nandonde. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, Renata Mzinga alisema ajali hiyo  ilitokea jana saa 11.30 alfajiri. Gari hilo lilikuwa likitoka mkoani Mtwara  kwenda Nachingwea. 

Aidha Kamanda huyo alitaja waliojeruhiwa ambao ni askari wa JWTZ kuwa ni  Simon Edward, Feruzi Hadji, Omary Makao, Mbaruku Duchi, Simon Masele,  Shadhili Nnandonde na mwingine aliyefahamika kwa jina moja Ndekenya.
Posted by MROKI On Wednesday, September 10, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo