Nafasi Ya Matangazo

November 05, 2011

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, akipokea zawadi ya Cd za kundi la T-Moto, kutoka kwa Mkurugenzi wa kundi hilo, Amin Salmin, baada ya Mama Zakhia kuzindua rasmi kundi hilo jana usiku kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee. 
Mgeni Rasmi Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, akizungumza jukwaani baada ya kuzindua rasmi kundi na albam ya kwanza ya kundi jipya la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) uzinduzi uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana Usiku Nove 4,2011. 
Mama Zakhia Bilal, Mama Tundu Pinda, Mama Kawawa, wakiwa katika picha ya pamo wasanii wa kundi la T-Moto baada ya kuzinduliwa rasmi.
Msanii wa kundi la Tanzania Modern Taarab, Mosi Suleiman, akiimba jukwaani wakati wa uzinduzi wa Kundi na albam ya kwanza ya kundi hilo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam jana usiku Nov 4.
Mkurugenzi wa Kundi la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) ‘Real Madrid’, Amin Salmin, akizungumza jukwaani wakati wa uzinduzi wa kundi hilo, uliofanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Posted by MROKI On Saturday, November 05, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo