Nafasi Ya Matangazo

November 04, 2011

Mkurugenzi wa kikundi cha muziki wa taarab  cha Zanzibar One,Abdulla Ali (DUU) akimakabidhi Cd za nyimbo mpya  za kikundi hicho,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,zilizopigwa katika Ukumbi wa Salama Bwawani,wakati wa kumpongeza kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kushika nafasi ya Urais wa Zanzibar.
Kikundi cha Culture Musical Club,kikitumbuiza  kwa nyimbo mbali mbali wakati wa kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kushika nafasi ya Urais wa Zanzibar,huko ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar juzi.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,na Mke wa Makamo wa Pili wa Rais,Mama PIli Balozi Seif,pamoja na wapenzi wa chama cha mapinduzi wakicheza Taarab wakati wa kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kushika nafasi ya Urais wa Zanzibar,juzi katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini  Zanzibar.
Mwimbaji wa Kikundi cha Calture Musical Club,Sabrina Hassan, akiimba wimbo wa Rais tunakusifu,wakati wa sherehe za kumpongeza Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,
Mwimbaji Makame Faki (sauti ya zege) wa Culture Musical Club,akiimba wimbo wa "Vyako wewe vya Mpeta"
Mwimbaji Makame Faki (sauti ya zege) wa Culture Musical Club,akiimba wimbo wa "Vyako wewe vya Mpeta"
 Wakazi wa Zanzibar waliohudhuria hafla hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Vuai Ali Vuai,Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,(wa pili kulia)na Mke wa Makamo wa Pili wa Rais,Mama PIli Balozi Seif,pamoja na wapenzi wa CCM Zanzibar  wakiangalia burudani ya muziki wa Taarab ya Vikundi tofauti vya musiki huo,vilivyoburudisha katika sherehe za CCM kwa kumpongeza Rais,kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kushika nafasi ya Urais wa Zanzibar,huko ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar juzi.
Posted by MROKI On Friday, November 04, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo