Nafasi Ya Matangazo

March 02, 2010

Mwimbaji wa mashujaa Band, German (kulia) akiimba wakati wa Onyesho katika ukumbi wa Makumbusho juzi.
Jado Fidifoce mbele wa bendi ya Mashujaa, akiongoza kucheza Sebene wakati walipotumbuiza katika ukumbi wa Makumbusho juzi.
Flora Bambucha wa Mashujaa Band(kulia) wakati wa onyesho katika ukumbi wa makumbusho mwishoni mwa juma.

Ikiwa ni siku chache tu tangu kundi ili la muziki wa dansi la Mashujaa Band liingie vitani katika medani ya Muziki, wimbo moshi wa sigara uliotungwa na Pansia Budansi umeanza kuwa gumzo kutokana na kuwa na mvuto kwa mashabiki na wapenzi wa muziki kote nchini.

mwishoni mwa juma band hiyo iliweza kufanya onesho lake katika ukumbi wa Makumbusho kabla ya jumapili kuamia katika ukumbi wake wa nyumbani wa mashujaa pub, ambako ukweli ni kwamba hadi mashabiki wa muziki kutoka mataifa mengine waliofika katika burudani kwa siku hizo waliwezaa kuisifia bendi hiyo na kusema kuwa vijana wakaze buti kwani inaweza kuwa tishio kwa bendi nyingine ndani nan nje ya nchi

aidha wanamuziki Jado Fidifoce, Germani, Pansia Budansi, ambao kwa hakika wanaonesha ukomavu wao katika fani hii, kwa upande wao wamewataka wapenzi kufika kwa wingi kupata burudani ambapo siku ya ijumaa wiki hii bendi hiyo itakuwa katika ukumbi wa Msasani klabu kuanzia saa tatu mpaka kucha.

kiongozi wa kundi hilo la muziki ELYSTONE ANGAI, amehaidi mambo makubwa kwa mashabiki ambapo amesema kuwa wafike siku zote waweze kuona vitu vipya kutoka kwao

"wapenzi wetu waje waone, hii ni bendi mpya ambayo imekuja na mambo mapya, na burudani zote ni mpya hivyo mashabiki wetu waje kusikia na kuona Moshin wa Sigara ulivyo" alisema angai

msemaji wa bendi hiyo Shaaban Mpalule, alisema kuwa maandalizi na shughulin zote kwa ajili ya kufanya maonyesho mengi zaidi kwa wiki yanaenelea,

"kikubwa tumejipanga kuwa na maonyesho matano kila wiki kabla ya kuhamia mikoani ambako pia baadhi ya mashabiki wameanza kuomba kwenda kupatriwa huduma ya burudani, ila kwa sasa bado tunashambulia katika majukwaa ya jijini ikiwa ni katika kumbi mbali mbali za burudani, mashabiki wafike kushuhudia bendi hii mpya ilivyokuja na vitu vipya, pia ina mvuto wa wanamuziki wote, viingilio vyetu ni vya hali ya kawaida inayomuwezesha kila mmoja kuingia ukumbini" alisema mpalule

mwishoni mwa juma yaani siku ya jumamosi ilitumbuiza katika ukumbi wa kijiji cha Makumbusho, jumapili ikashusha burudani katika ukumbi wake wa nyumbani wa Mashujaa Pub uliopo Vingunguti jijini Dar es Salaam.

aidha uongozi unajipanga ili uweze kuwatangazia ratiba ya kila wiki kuanzia siku ya jumatatu hadi jumapili.

wote mnakaribishwa.
Posted by MROKI On Tuesday, March 02, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo