Nafasi Ya Matangazo

March 24, 2010

Miss Universe Tanzania 2009, Iluminata James akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ua uzinduzi wa mashindano ya mwaka huu ya kumtafuta Miss Universe Tanzania jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Ofisa Uhusiano wa Serengeti Breweries, Imani Lwiga na Mkurugenzi wa Compass Communications, Maria Sarungi.
Ofisa Uhusiano wa Serengeti Breweries, Imani Lwiga (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shs milioni 12 kwa Mkurugenzi wa Compass Communikcations, Maria Sarungi ikiwa ni sehemu ya udhamini wa kampuni hiyo katika mashindano ya Miss Universe Tanzania 2010 wakati wa hafla ya uzinduzi wake kwenye Hoteli ya Moevenpick Royal Palm jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni mrembo anayemaliza muda wake, Iluminata James. Meneja Masoko wa Precision Air, Emilian Rwejuna (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu udhamini wao katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Universe Tanzania 2010 katika hafla ya uzinduzi wa mshindano ya mwaka huu kwenye Hoteli ya Moevenpick Royal Palm jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa PSI, John Wanyancha na Meneja Mauzo na Masoko wa Moevenpick, Zena Sapi ambao wote ni wadhamini wa mashindano hayo.
Posted by MROKI On Wednesday, March 24, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo