Nafasi Ya Matangazo

December 02, 2008

Katuni za King Kinya katika Treni ya ardhini huko Berlin Ujerumani
Mdau Francis Chokara wa Ujerumani amenitumia ujumbe huu wa pongezi kwa King Kinya na picha hizo hapo juu.

From: francis chokara <frachoma1@yahoo.com>
Subject: HONGERA KING KINYA
To: "mroki" mrokim@gmail.com
Date: Monday, 1 December, 2008, 6:34 PM

Ndugu yangu habari za kazi ngumu za kila siku kutupa habari nyingi za hapo nyumbani. Mimi ni mpenzi mkubwa sana wa Blog yako, nafurahishwa sanana kazi zako. Hongera sana kwa kazi nzuri unayoifanyakutupa habari ndugu zako.Siku ya Tarehe 2-11-2008, hapa Berlin, kwenye treni zachini ya ardhi nilipata bahati ya kuona katuni ya Mtanzaniamwenzetu King Kinya ndani ya treni,kila alieiona alifurahishwa na katuni hii. Nimeonanimpongeze King Kinyakupitia Blog yako, ajue na pia kuwapa moyo wachorajikatuni wote Tanzania wajue kazi zao nzuri huwa zinaonyeshwahapa Berlin. Ongezeni bidii wachoraji wote ili mjulikanekimataifa, hii ni kazi ya pili sasa ya Mtanzania kuionakatika treni hizi. Hapo mwanzo niliona kazi ya Ally Masoud(Kipanya) Bahati mbaya sikupata picha yake. Nawatakia afyanjema na kila la kheri wote, ni mimi mpenda maendeleo yaWatanzania wote.
Posted by MROKI On Tuesday, December 02, 2008 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo