Makamu wa Rais, Mhe.
Deogratius Ndejembi, ametoa wiki mbili kwa Wizara ya Mipango, Kilimo na Fedha
kuandaa mpango wa mafunzo kwa vitendo utakaowapa angalau vijana 10,000 fursa
katika Taasisi na Mashirika ya Umma ya Kufanya mafunzo kwa Vitendo huku wengine
20,000 wakilengwa katika sekta binafsi.
Akizungumza Arusha wakati
akimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi cha
Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma C-CEOs Forum 2026.
Makamu wa Rais, amesema mpango huo utawajengea vijana uzoefu wa kuajirika na
kujiajiri, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Dira 2050.
Aidha, ameyataka Mashirika ya
Umma kuwa injini ya mageuzi ya uchumi, kuongeza tija, kubana matumizi yasiyo ya
lazima na kuhakikisha uwekezaji wa Serikali unaleta matokeo yanayogusa maisha
ya wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







0 comments:
Post a Comment