Nafasi Ya Matangazo

September 15, 2026

Wahiutimu wa Mafunzo ya vijana ya Kujitolea Op Nishati Safi pamoja na Op Linda Amani ( Mujibu wa Sheira) wakifanya gwaride lao maalum la kuhitimu mafunzo katika viwanja vya Gwaride vya JKT Makutupora Mkoani Dodoma Septemba 14,2026.

Mwakilishi wa Mkuu wa JKT, Brigedia Jenerali Shija, akitoa salam za jeshi hilo wakati wa kufunga mafunzo kwa Mafunzo Vijana wa JKT kwa Mujibu wa Sheria  OP Linda Amani katika Kambi ya JKT Makutopora Mkoani Dodoma Septemba 14,2026. 
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Thobias Nyingo, akihitimisha Mafunzo Vijana wa JKT kwa Mujibu wa Sheria  OP Linda Amani katika Kambi ya JKT Makutopora Mkoani Dodoma Septemba 14,2026. 
*************
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Thobias Nyingo amempongeza Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi anavyoendelea kuweka Mkazo katika Mafunzo ya Jeshi hususan kwa Mafunzo ya Vijana kwa Jeshi la Kujenga Taifa.
Hayo ameyasema leo wakati akihitimisha Mafunzo ya vijana ya Kujitolea Op Nishati Safi pamoja na Op Linda Amani ( Mujibu wa Sheira) katika viwanja vya Gwaride vya Makutupora JKT .
Aidha amewakumbusha Wananchi wote waliohudhuria hafla hiyo na hata Vijana waliohitimu Mafunzo hayo juu ya tahadhari ya kuwepo kwa Mvua kubwa ya Elnino inayoweza kutokea katika ardhi ya Tanzania vivyo amewaasa wananchi kutunza Chakula, na kuzibua mitalo.
Nae Mwakilishi wa Wa Mkuu wa Majeshi ambae pia ni Mkurugenzi wa Mipango Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Brigedia Jenerali Gerald Omari amempongeza Kamanda Kikosi na Wakufunzi wote kwa jinsi walivyoweza kutoa mafunzo kwa Vijana kwani Vijana hawa wametoka pande tofauti tofauti za nchi ya Tanzania.
Akitoa salamu za Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Shija Lupi, amewataka vijana hao kwenda kuwa mabalozi wa JKT.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Thobias Nyingo, akikagua gwaride maalum la kufunga mafunzo ya vijana wa JKT Makutopora. 

Mwandishi Patricia Kimelemeta (kulia), akibadilishana mawazo na watoto wake mapacha Kulwa na Doto baada ya kuhitimu mafunzo ya awali ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) 834 Makutupola OP Linda Amani  kwa upande wa mujibu wa sheria na Operesheni Nishati safi kwa upande wa kujitolea. Sherehe hizo zimejumuisha maonyesho mbalimbali na uonyeshaji wa morali na uzalendo wa vijana hao waliohitimu mafunzo yao katika kikosi hicho kilichopo mkoani Dodoma.






Posted by MROKI On Tuesday, September 15, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo