WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza wakati wa ufuinguzi wa Mkutano wa mwaka wa vyombo vya utangazaji nchini uliondaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) mjini Dodoma.
Na Eugenia Kimolo, Dodoma
Na Eugenia Kimolo, Dodoma
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi amewaonya watangazaji wa vyombo vya habari kuacha kubananga umma kuhusu Matumizi sahihi ya lugha Kiswahili.
Akizungumza jijini Dodoma Leo kwenye Mkutano wa mwaka wa vyombo vya utangazaji nchini uliondaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Professa Kabudi amesema baadhi ya watangazaji wamekuwa wakipotosha umma kwa kutamka matamshi yasiyo sahihi akitolea mfano apa badala ya hapa, uyu badala ya huyu huku ni kupotosha wananchi.
"Tanzania tumefubaza Kiswahili kwa kudumaza kwa maneno kadhaa, kubananga Kiswahili matokeo yake watumiaji wengine wa nchi zingine wanaona hatuzungumzi kwa ufasaha, "Watangazaji mna jukumu la kuhakikisha mnatangaza kwa lugha fanisi na fasaha.
Vyombo vya Habari mna mchango mkubwa wa kusahihisha makosa mkiendelea hivyo, hilo ni janga litaigharimu nchi na kuacha kuwa kinara"alisema.
Amezitaka mamlaka zinahusika kuwachukulia hatua watangazaji ambao hawazingatii maadili ya matamshi ya Lugha fasaha ya Kiswahili.
Pia, amewataka wamiliki wa vyombo vya habari kuweka vipindi vya kuelimisha kwa wingi kuliko kuweka burudani na michezo kwa muda mwingi na kuwachukulia hatua watangazaji ambao hawawezi kutamka kiswahili kwa ufasaha.
0 comments:
Post a Comment