Nafasi Ya Matangazo

July 15, 2024

Mbunge wa jimbo la Newala Mjini na Waziri Ofisi ya Rais Kazi Maalum Mhe. George Mkuchika akizungumza katika Moja ya mikutano yake.
Mbunge wa jimbo la Newala Mjini na Waziri Ofisi ya Rais Kazi Maalum Mhe. George Mkuchika amefanya ziara katika jimbo lake la Newala Mjini na kuwahiza wananchi kujitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa huku akisisitiza serikali ya kijiji inatakiwa kuwa na viongozi mchanganyiko.

Ameyasema hayo Julai 13, 2024 katika mikutano tofauti ya siku yake ya kwanza katika kata ya Julia, Makote na Mahumbika ambapo ameeleza kuwa serikali ya kijiji haitakiwi kuwa wazee peke yao, au vijana peke yao au wamawake peke yao bali kuwe na mchanganyiko wa viongozi kutoka makundi yote.

“Tujitokeze kugombea, lakini baba wa taifa alitufundisha unapofika wakati wa uchaguzi ukiona mtu fulani anafaa umshawishi achukue fomu, nyie akina mama mkimuona wakutuwakilisha akimama fulani anaweza mshawishi achukue fomu”. Amefafanua Mhe. Mkuchika.

Aidha Mbunge Mkuchika amewaomba wananchi kuanza katika hatua ya kujiandisha ili waweze kutumia haki yao ya kushiriki uchaguzi huo kwa kugombea au kuchagua kiongozi anayefaa “siku ya kupiga hautaweza kupiga kura kama haujajiandisha, itabidi wewe ukubali matokeo ya kura za wenzako”.

Katibu wa siasa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Newala Ndg. Shazili Nambaila amewasisitiza wanachama wa chama hicho kuwa mstari wa mbele katika kujiandisha wakati utakapofika ili chama kiweze kuendelea kupata matokeo bora kutokana na idadi ya wananchama waliojiandikisha.

Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji Newala Bi. Hajara Napinda amewataka watu kuwa tayari kwa zoezi la kuboresha taarifa kwenye daftari la mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa litakaloanza tarehe 11/10/2024 mpaka tarehe 20/10/2024.

Aidha Napinda amesisitiza kuwa nafasi ya kuboresha daftari ni muhimu kwa kila mwananchi, itampa sifa ya kuwa mshiriki wa uchaguzi na kuchagua viongozi watakao simamia dira ya maendeleo ya vijiji na mitaa kwa miaka mitano ijayo.

Tanzaniahufanya uchaguzi wa serikali za mitaa kila baada ya miaka 5 na uchanguzi wa mwisho ulifanyika mwaka 2019 hivyo mwezi Novemba mmwaka2024 unatarajiwa kufanyika uchaguzi mwingine. 

Posted by MROKI On Monday, July 15, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo