Nafasi Ya Matangazo

September 16, 2024


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

 (i)  Bi. Nenelwa Mwihambi ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu, Bi. Mwihambi alikuwa Katibu wa Bunge; na

(ii) Bw. Baraka Ildephonce Leonard ameteuliwa kuwa Katibu wa Bunge. Bw. Leonard anachukua nafasi ya Bi. Mwihambi ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Viongozi walioteuliwa wataapishwa tarehe 19 Septemba, 2024 saa 09.00 alasiri, Ikulu – Dar es Salaam.

Posted by MROKI On Monday, September 16, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo