Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule leo tarehe 16 Disemba 2023 ameshiriki zoezi la kufanya usafi wa mazingira na wananchi wa jiji la Dodoma katika maeneo ya mailimbili,Mipango na Mzakwe.
Akizungumza katika zoezi hilo Mhe. Senyamule ameagiza kwa kila mwananchi kuwa na tabia ya kuchukia uchafu katika mazingira yanayowazunguka ili kuepukana na Magonjwa ya miripuko.
“Kila mtu anahaki ya kutunza mazingira ili kuepuka uchafuzi wa mazingira katika maeneo tofauti tofauti kwa kuwa mlinzi wa mazingira katika kuyatunza.
“Viongozi wetu chini ya Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan wamekuwa vinara namba moja katika kuhamasisha usafi wa mazingira, vile vile madereva wa mabasi hakikisheni mnakuwa na kibebea taka katika vyombo vya usafi vinavyopita hapa Dodoma kwa sababa hii ni makao Makuu hivyo hata mazingira yawe na hadhi yake."Amesema Senyamule
Kwa Upande Wake, Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma jiji Ndg.Sakina Mbugi amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kusimamia maeneo yote ambayo bado yapo katika hali ya uchafu kuweka mikakati ili kuhakikisha mazingira yanakuwa katika hali nzuri.
0 comments:
Post a Comment