Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amewataka wanawake wa Dodoma kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo mkoani hapo ili kujiinua zaidi.
Mh Mavunde ameyasema hayo jana wakati akiongea na wakina mama wajasiriamali wa Dodoma ambao walikuwa wakisheherekea miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa US AS ONE-KICOBA.
“Ninawapongeza sana kwa muunganiko huu wenye dhamira ya kuinuana kichumi kupitia VICOBA.
Kwa miaka mitatu tangu kuanzishwa kwenu mmepiga hatua na kupata mafanikio makubwa ikiwemo kuongeza mtaji mpaka kufikia 63m.
Serikali chini ya uongozi wa Mh Rais Dkt. Samia SuluhuHassan imefanya kazi kubwa ya kuweka mazingira rahisi ya uwekezaji Jijini Dodoma na hivyo kuongeza wigo mpana wa kiuchumi.
Hivyo nitoe rai kwenu kutumia fursa hii kubwa kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili kujiongezea kipato na kukuza uchumi wenu,kama Mbunge wenu nitakuwa tayari kuwashika mkono na kuwaongoza vyema”Alisema Mavunde
Akisoma risala,Mwenyekiti wa US AS ONE-KICOBA Bi. Pauline Chuma* amesema madhumuni yao hivi sasa ni kukua kutoka KICOBA kwenda kuwa SACCOS ili kutanua wigo wa shughuli zao sambamba na kuongeza idadi kubwa ya wanachama ili kuunganisha nguvu kwa pamoja.
Akitoa shukrani kwa niaba,Katibu wa US AS ONE-KICOBA amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kukubali ombi lao la kuwa Mlezi wao pamoja na kuwachangia Tsh 3,000,000 za ununuzi wa vifaa vya kupikia.
0 comments:
Post a Comment